Jumamosi, 30 Mei 2015

JEEE!!!! UNAZITAMBUA SIFA ZA MPENZI WA KWELI. HIZI NI SIFA KUMI KATIKA SIFA MOJA WAPO



Ukweli ni kwamba vijana wengi ambao wanapendana leo, mapenzi yao hayadumu kiasi cha kubatizwa jina la utamu wa banzoka. Lakini yote hii inatokana na ukweli kwamba elimu ya mapenzi ambayo ni muhimu kwa binadamu haitolewi ipasavyo.
Ipo dhana potofu kwamba kumfundisha mtoto mapenzi ni kumharibu, jambo ambalo si kweli bali inategemea mtoto huyo anafundishwa nini na kwa wakati gani.
Lakini cha kushangaza zaidi hata watu wazima ambao ni wadau wa mapenzi hawayajui matokeo yake wanajiingiza kwenye uhusiano wakiwa bumbumbu na hivyo kuteswa na changamoto zinazowakabili ndani yake.
Leo tutajifunza kwa undani sifa kumi za mpenzi bora ili tuweze kuwatambua wapenzi wetu kabla ya kuwapa mioyo na utu wetu. Twende tukaone.1. Mpenzi wa kweli ni yule ambaye hatangoja kujua nini unahitaji yaani hana sababu ya kusubiri kuombwa ndiyo atoe msaada.
Kwa kuwa ana mapenzi ya dhati na anajua mahitaji yako, hawezi kusubiri kushurutishwa au ionekane kama vile anatoa hongo. Kipengele hiki kinawahusu wanaume zaidi.
2. Ni yule atakayejua wakati gani huna furaha au una furaha na atakuwa na wewe kwa hali zote mbili. Hata kama ukiwa huna furaha, hujiona mwenye jukumu kuhakikisha unakuwa nayo kwa namna yoyote ile.


3. Ni yule atayekuwa tayari kukusikiliza kwa kile utakachosema, hatajali umezungumza baya au zuri. Kwa bahati nzuri ni kwamba, ikiwa umekosea, yeye atachukua jukumu la kukuweka sawa.
Asiye na penzi la dhati, ukikosea kwake ni kichekesho. Badala ya kukurekebisha na kukuweka kwenye mstari, atakucheka.
4. Atakuwa na wewe wakati wa shida na raha. Hatakuwa mtu wa kuviziavizia na kujisogeza wakati ukiwa na raha.Kwake, shida yako itakuwa yake akiwa na imani kuwa, hata yake ni yako pia. Anayejiweka kando ukiwa na matatizo, siyo sahihi, mwepuke.
5. Mpenzi wa kweli atakuheshimu na hatapenda kuwa kikwazo cha maisha yako, atakulinda daima. Heshima ni msingi mkuu.
6. Atakupenda kwa moyo wake wote na wala si kwa ajili ya shinikizo fulani. Pesa si kipaumbele chake.
7. Mpenzi wa kweli ni yule atakayeonyesha kuthamini nafasi yako kama rafiki au mpenzi mbele ya wengine, hafichi hisia zake mbele za watu, atakutetea na kukufanya wa kwanza.
8. Kwenye ukweli mpenzi mzuri atasema bila kukuficha na atapenda kukuonyesha mifano ya namna ya kuwa mkweli na mwaminifu.
9. Mpenzi wa kweli ni yule anayejiamini, asiyeyumba katika maamuzi hata kama atalazimika kufanya maamuzi magumu.Kikubwa ni kusimamia katika ukweli na masilahi yanayoeleweka.


10. Atakuwa tayari kuvumilia, hatakuwa mwepesi wa hasira wala kutumia lugha chafu na ubabe. Ni mwelekezaji zaidi, hawezi kukurushia maneno ya kuudhi maana anajua kukuudhi au kukuumiza ni kuharibu maana nzima ya penzi lenu.Bila shaka vipengele hivyo vimekubadilisha sana

Ijumaa, 29 Mei 2015

MPENZI WAKO NA UNATAKA KUUTIBU?


USIDANGANYIKE rafiki yangu, ukitaka kuwa bora katika jambo fulani lazima ukubali kujifunza kila siku. Hata kama unajiamini kiasi gani, toa nafasi kwa ubongo wako ili uweze kuingiza vitu vipya.
Naam! Hapa kwenye All About Love ndiyo sehemu sahihi zaidi ya kuongeza ujuzi wa mambo ya saikolojia ya uhusiano. Ninao marafiki wengi sana ambao wamekuwa nami kwa muda mrefu sasa katika gazeti hili na lingine la Ijumaa ambayo kwa hakika yameendelea kuwa mwalimu wao kwenye uhusiano.

Hebu sasa tabasamu, maana leo unakwenda kujifunza kitu kipya kabisa. Hutakuwa kama ulivyo sasa mara baada ya kumaliza kusoma mada hii. Karibu sana rafiki yangu.
Katika mapenzi ni jambo la kawaida kabisa kugombana na kufikia hatua ya kutengana kwa muda. Naomba hapa niweke wazi kitu kimoja, nazungumzia zaidi kwenye uhusiano wa mapenzi, kabla ya ndoa. Nazungumza na wachumba zaidi.




Inawezekana kukawa kumetokea kutokuelewana baina yenu, mkaachana. Ukiwa nje ya uhusiano wako, ukagundua kwamba chanzo cha matatizo yote ni wewe. Inategemea umemfanyia nini? Labda umemtukana sana, umeharibu samani zake nk, lakini mwisho wa siku unagundua kwamba wewe ni chanzo cha matatizo hayo ya kutengana.

Kama kweli mna mapenzi ya dhati, mnaweza kukutana na kujadiliana pamoja, halafu mwisho wa siku mkajikuta mmeamua kurudiana. Hakuna makosa katika hilo.
Kinachowarudisha pamoja ni mapenzi ya dhati pekee na si kitu kingine chochote, lakini pamoja na penzi hilo, unatakiwa kufahamu kwamba mwenzako atakuwa na majeraha ndani ya moyo wake, atakuwa na vidonda ambavyo vinapaswa kuwekewa dawa ili apone kabisa!
Mwenye wajibu wa kumwekea dawa ni wewe mwenyewe! Kabla ya kufika huko, soma kwanza kipengele kinachofuata.

KUJERUHI NI KUPI HASA?
Maneno yako makali, tabia zako mbaya, vituko vya kila aina na hasara ulizomsababishia, zinaweza kuwa sababu ya kumjeruhi moyo wake. Majeraha pia yanaweza kusababishwa na jinsi usivyo msikivu kwake, wakati akiwa anaamini kwamba wewe ndiye mpenzi wa maisha yake yote.
Sawa, ameamua kurudiana na wewe, kwasababu anakupenda lakini bado anahisi kama utaendelea na matatizo yako ya zamani. Hakuamini. Anaona anaweza kuwa anatwanga maji kwenye kinu, ambapo ukweli ni kwamba mwishowe maji yote yatamwagika chini.

UTAJUAJE KAMA UMEMJERUHI?
Yapo mengi, lakini kwa uchache sana, atapunguza mahaba na wewe. Ninaposema mahaba sina maana ya ngono, namaanisha mambo ya kimapenzi – mahanjam - manjonjo.
Anakuwa mgumu kupokea simu yako, hata akipokea hazungumzi maneno ya kimahaba kama zamani. Ukimwambia: “I love you dear,” yeye anaweza kukujibu kwa kifupi: “Ahsante,” tofauti na zamani ambapo alikuwa akikujibu kwa mahaba mazito: “I love you too my sweetie.”
Meseji zako hajibu, hata kama akijibu, atakujibu kwa mkato sana. Anaonekana hana msisimko na wewe. Atakuwa mzito hata kuachia tabasamu akizunguza na wewe, hakuamini sana.
Hakufuatilii sana, mara nyingi anaonekana mwenye mawazo mengi akiwa na wewe. Hafurahii anapokuwa na wewe na hata uchangamfu wake unapungua.
Kikubwa hapo ni kwamba hana imani kama ni kweli umeamua kwa dhati kubadilika na kurudi kwake mzima-mzima! Moyo wake unaendelea kukiri ndani kwamba anakupenda, lakini anashindana na imani kwamba yawezekana usibadilike, anachohofia yeye ni wewe kurudia makosa yale yale!
Kama ukiona dalili zote hizo ujue wazi kwamba bado ana wasiwasi na wewe, moyo wake umejeruhiwa. Kufahamu ni hatua ya kwanza, nzuri na muhimu sana kwako, kwani angalau sasa utakuwa unajua upo kwenye uhusiano na mtu wa aina gani, huku ukiwa makini katika kutafuta suluhisho la tatizo lenyewe.

ONESHA UNAFAHAMU
Kitu cha kwanza kabisa unachotakiwa kufanya ni kuonesha kwamba umeshafahamu kwamba hakuamini na hana msisimko tena na wewe. Unatakiwa umfanye ajue kwamba unatambua kinachendelea, lakini unakiri kwamba ni haki yake kufanya hivyo, maana ni kweli kwamba mkosaji ulikuwa ni wewe.




ACHA KUMLAUMU...
Katika makosa makubwa ambayo hutakiwi kufanya ni pamoja na kumlaumu! Hutakiwi kabisa kumlaumu kwamba anakosea kufanya anavyofanya. Lakini kwa vitendo, unatakiwa kuanza kubadilika taratibu huku ukionesha kumhurumia kwa hali aliyokuwa nayo.
Bado kuna vipengele vingine muhimu sana kwako kuvifahamu wakati unapofanya jitihada za kumrudisha mpenzi wako katika hali yake ya kawaida. Kumbuka, wewe ndiye uliyeharibu, hivyo ni wajibu wako kutengeneza. Wiki ijayo tutaendelea, USIKOSE!



Jumanne, 19 Mei 2015

Kutana na ngoma inayo hit bongo

Ki ukweli Baraka Da Prince amenogeza Mapenzi ya watu Fulani hivi kutokana na hii nyimbo kugonga nyoyo zao,....